Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 11
Maneno ya Baba Mtakatifu Fransisko
Kanisa lazima lijitokeze nje. Kwenda wapi? Kwa viunga vya maisha,
chochote kinachoweza kuwa, lakini lazima litoke nje. Yesu anatuambia,
“Enendeni ulimwenguni mwote! Nenda! Hubiri! Shuhudia Injili! ”
Ninapendelea sana Kanisa ambalo limepata ajali chache kuliko Kanisa
ambalo limegonjeka kutokana na kufungwa. Toka nje, toka nje! ... ni
mara ngapi Yesu yu ndani na kugonga mlango ili atolewe, atoke? Na
hatumruhusu atoke nje kwa sababu ya hitaji letu binafsi la usalama… ’
(Baba Mtakatifu Fracisko, Kanisa la Huruma, uk.99)
Tafakari
(Itolele na msemaji , Padri, shemasi, watawa au walei)
Mda wa kutafari
Injili Takatifu :Somo (Lk 1:46-55)
Simameni
Kiongozi:
Wote:
Tubu
Na kuamini injili
Kushoto:
Mwoyo wangu † wantukuza Bwana,
roho yangu inamshangilia Mungu Mwokozi
wangu;
kwa kuwa ameutamaza Unyonge wa Mjakazi
wake.
Kulia :
Kwa maana tazama tokea sasa vizazi wote
wataniita mbarikiwa. Kwa kuwa wenye Nguvu
amenitendea makuu, na jina lako ni takatifu.
Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwa
hao wanamcha
Kushoto:
Umeonyesha nguvu kwa mkono wako
na kuwatawanya wenye kiburi katika mawazo ya
mioyo yao,
Amewaangusha wakuu katika viti vya vya enzi;
Wiki ya Kwana - Jenga Kanisa langu upya
11