Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 12
Kushoto:
na wayonge amewakweza.
Wenye njaa amewashibisha mema,
na matajari amewaondoa mikono mitupu.
Kulia:
Umemsaidia mtumishi wako, Israeli,
Ili kukumbuka rehema zake,
Kama alivyowaambia baba zake,
Ibrahimu na uzao wake hata milele.
Wote:
Atakuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,
kama mwanzo, hata sasa, na siku zote, milele.
Amina.
Tubuni na kuiamini injili.
Sala ya Waumini
Kiongozi:
Wote:
12
Tuombe kwa Mwokozi wetu, Yesu Kristo, aliye
tufanya kuwa mwili wake;
tutakase na Neema yako ya Kimungu ili tuwe
watakatifu wako
Kiongozi:
Wote:
Yesu, jiwe kuu la pembeni la Kanisa lako;
Fanya wote waliobatizwa kuwa mawe hai, ili
tukineemeshwa na tamaduni na mila zetu Watu wa Kwanza taifa hili, wazao wa walowezi
wa Uropa, wahamiaji na wakimbizi - tuliunde
hekalu la kiroho katika Roho Mtakatifu
Kiongozi:
Wote:
Yesu, Mchungaji Mwema wa Kanisa lako;
Tuchunge, utulinde na utuongoze katika njia ya
mapito yako.
Kiongozi:
Wote:
Yesu, Msamaria Mwema;
wabariki wote waliojeruhiwa na dhambi na
kuumizwa na majanga ya maisha, waponye kwa
zeri ya Roho Mtakatifu.
Sala za Jioni za Kwaresma 2021