Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 13
Kiongozi:
Wote:
Yesu, Bwana na Mwalimu;
tujalie kulisikiliza kwa makini neno lako, kama
Mama yako, Mariamu, ili tuweze kulitafakari
katika mioyo yetu na ili tujifunze jinsi ya
kulijenga Kanisa lako upya.
Kiongozi:
Wote:
Yesu, Njia, Ukweli na Uzima;
kusanya kwako katika maisha ya milele wale
wote wanaotafuta kuishi kwa ukweli wako,
wakikufuata siku kwa siku.
Kiongozi:
Tukiyafuata mafundisho ya Yesu, kama Kanisa
tukitafuta upya, tunaomba:
Baba yetu…
Wote:
Sala
Kiongozi:
Wote:
Tujalie, Mwenyezi Mungu,
kupitia maadhimisho ya kila mwaka ya Kwaresima
takatifu, tunaweza kukua katika ufahamu wa
utajiri wa neema uliofichwa ndani ya Kristo
na hivyo kujenga upya hicho kilichovunjika katika
Kanisa letu na maishani mwetu.
Kwa njia ya Mwanao Bwana wetu Yesu Kristo
Amina
Wiki ya Kwana - Jenga Kanisa langu upya
13