Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 14
Baraka
Tupige magoti
Padri / shemasi huenda kwenye altari, huinama na kupiga magoti. Wakati
wimbo unaozingatia Kristo unaimbwa, muhudumu, bado anapiga magoti,
hufukia ubani Sakramenti kuu katika monstransi. Kisha anainuka na kusema:
Waziri:
Wote:
Tuombe:
Bwana Yesu Kristo,
ulitupa Ekaristi Takatifu
kama kumbukumbu ya mateso na kifo chako.
Tunapoiabudu Sakramenti hii ya mwili na damu
yako
tujaliwe kupata wokovu uliotushindia
na amani ya ufalme
unayeishi na Baba na Roho Mtakatifu,
Mungu, milele na milele.
Amina
Baada ya sala muhudumu huvaa pazia la humeral, huinama, na kuchukua
monstransi. Kwa ukimya anafanyia watu Ishara ya Msalaba na monstransi.
Sakramenti Kuu huchukuliwa kutoka kwa monstransi na kuekwa katika
Tabanako takatifu.
Mwisho
14
Kiongozi:
Wote:
Bwana awe nanyi
Awe pia nawe.
Kiongozi:
Wote:
Nendeni na amani ya Kristo
Tumshukuru Mungu.
Wote wanasimama
Sala za Jioni za Kwaresma 2021