Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 18
Kiongozi:
Wote:
Yesu, nuru ya Mungu inayong’aa;
tuondolee giza la dhambi na tamaa inaoshika
ulimwengu wetu katika utumwa, tufanye huru
kwa sifa na utukufu wa jina lako takatifu.
Kiongozi:
Wote:
Yesu, mnyenyekevu na mpole wa Moyo;
Pokea kwako wote waliolishwa kwa neno lako, ili
waweze kujazwa na upendo wako wa milele.
Kiongozi:
Yesu alituonyesha kwamba Baba yake ni Baba yetu
pia; hivyo basi tuombe:
Baba yetu…
Wote:
Sala
Kiongozi:
Wote:
Mwenyezi Mungu,
umetuamuru tumsikilize Mwanao mpendwa.
Kuwa radhi kutulisha ndani kwa neno lako,
ambalo, kwa macho ya mioyo yetu limewekwa
wazi,
tuweze siku moja kukutazama katika utukufu.
Kwa njia ya Bwanao, Yesu Kristo
Amina
Baraka
Wote Tupige magoti
Kasisi / shemasi huenda kwenye altari, huinama na kupiga magoti. Wakati
wimbo unaozingatia Kristo unaimbwa, muhudumu, bado akipiga magoti,
huifukia ubani Sakramenti Kuu katika monstransi.
Kisha anainuka na kusema:
18
Sala za Jioni za Kwaresma 2021