Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 21
Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko
Ketini
‘Kuwa rafiki na Mungu kunamaanisha kuomba kwa urahisi, kama watoto
wanavyowatumainia wazazi wao ... Yule anayesikiliza kwa makini neno la
Mungu na kuomba kweli, huuliza Bwana kila wakati:’ mapenzi yako ni
nini kwangu?’
(Papa Fransisko: Roho ya Mtakatifu Francisko:
Maneno ya kuhimiza juu ya imani, upendo na uumbaji)
Tafakari
(hutolewa na kasisi/msemaji /mgeni, mtawa au Mlei)
Tafakari kwa kimya
Injili takatifu: Somo (Lk 1:46-55)
Simameni
Kiongozi:
Wote:
Omba na utapewa; tafuta nawe utapata;
bisha na utafunguliwa mlango.
Kushoto:
Mwoyo wangu wantukuza Bwana,
roho yangu inamshangilia Mungu Mwokozi
wangu;
kwa kuwa ameutamaza Unyonge wa Mjakazi
wake.
Kulia :
Kwa maana tazama tokea sasa vizazi wote
wataniita mbarikiwa.
Kwa kuwa wenye Nguvu amenitendea makuu,
na jina lako ni takatifu.
Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwa
hao wanamcha
Kushoto:
Umeonyesha nguvu kwa mkono wako
na kuwatawanya wenye kiburi katika mawazo ya
mioyo yao, Amewaangusha wakuu katika viti vya
vya enzi; na wayonge amewakweza.
Wenye njaa amewashibisha mema,
na matajari amewaondoa mikono mitupu.
Wiki ya Tatu -Tufundishe Kusali
21