Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 22
Kulia:
Umemsaidia mtumishi wako, Israeli,
Ili kukumbuka rehema zake,
Kama alivyowaambia baba zake,
Ibrahimu na uzao wake hata milele.
Wote:
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,
kama mwanzo, hata sasa, na milele milele.
Amina.
Omba na utapewa; tafuta nawe utapata;
bisha na mlango utafunguliwa kwako.
Sala ya waumini
Kiongozi:
Wote:
Kiongozi:
Wote:
Kiongozi:
Wote:
22
Katika maisha yake yote hapa duniani, sala ilikuwa
ya kusuka sana kupitia maisha ya familia na jamii
ya Yesu, na pia katika huduma au utumishi wake
na katika kufa kwake;
sala iweze kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila
siku ili tuweze kufahamu kwamba tunaishi
katika uwepo wa Mungu.
Yesu, wakati wa maisha yako na Mariamu
na Yusufu, kama mtoto na kama kijana, sala
ilidumisha upendo na utii, na kujionyesha katika
hekima na ukomavu wako.
Fadhili familia zetu ziwe mahali ya sala, ili
katika kwenda kwetu nje na katika kurudi kwetu
nyumbani, tutampata Yesu mgeni wetu daima.
Kama familia, Yesu, ulikusanyika na Mariamu
na Yusufu na wanakijiji katika sinagogi kusikia
Maandiko, na katika Hekalu la Yerusalemu kutoa
dhabihu;
Fadhilia familia zetu kusali kifamilia na
kukusanyika na jamii kwa Ekaristi ya Jumapili,
ambapo dhabihu ya sifa hutolewa.
Sala za Jioni za Kwaresma 2021