Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 24
Baraka
Wote Tupige magoti
Kasisi / shemasi huenda kwenye altari, huinama na kupiga magoti.Wakati
wimbo unaozingatia Kristo unaimbwa, muhudumu, bado akipiga magoti,
huifukia ubani Sakramenti Kuu katika monstransi.
Kisha anainuka na kusema:
Muhudumu:
Wote:
Tuombe:
Bwana,
tupe mioyo yetu
mwanga wa imani na moto wa upendo,
ili tuabudu katika roho na kweli
Bwana na Mungu wetu , uliye katika sakramenti
hii, unayeishi na kutawala daima na milele.
Amina
Baada ya sala muhudumu huvaa pazia la humeral, huinama na kuchukua
monstransi. Kwa ukimya anawabariki watu kwa Ishara ya Msalaba na monstransi.
Sakramenti Kuu huchukuliwa kutoka kwa monstransi na kuekwa katika
Tebanako.
Mwisho
24
Wote wanasimama
Kiongozi:
Wote:
Bwana awe nanyi
Awe pia na nafsi yako.
Kiongozi:
Wote:
Nendeni kwa amani ya Kristo
Tumshukuru Mungu.
Sala za Jioni za Kwaresma 2021