Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 26
Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko
Wote wanaketi
Ishara ya Yesu kwenye karamu ya mwisho ni shukrani ya juu kabisa
kwa Baba kwa upendo wake, kwa huruma yake. Ekaristi ni kilele cha
ukombozi wa Mungu. Bwana Yesu, kwa kuwa mkate uliomegwa kwa
ajili yetu, tumiminie rehema zako zote na upendo wako, ili tuwe na upya
mioyoni mwetu, maishani mwetu na njia zetu za uhusiano naye na ndugu
zetu.
Tumwombe Bwana wetu atusaidie kutoa ushuhuda unaoangazia huruma
yake na upendo wake katika kila sehemu ya maisha yetu ya Kikristo.
(Papa Francisko: Hadhira kuu, Roma, Februari 2014)
Tafakari
(hutolewa na kasisi/msemaji /mgeni, mtawa au Mlei)
Tafakari kwa kimya
Injili Takatifu: Somo (Lk 1:46-55)
26
Wote wanasimama
Kiongozi:
Wote:
Mungu huwahurumia wale wanaomcha
Kizazi hata Kizazi.
Kushoto:
Mwoyo wangu † wantukuza Bwana,
roho yangu inamshangilia Mungu Mwokozi
wangu; kwa kuwa ameutamaza Unyonge wa
Mjakazi wake.
Kulia :
Kwa maana tazama tokea sasa vizazi wote
wataniita mbarikiwa.
Kwa kuwa wenye Nguvu amenitendea makuu,
na jina lako ni takatifu.
Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwa
hao wanamcha
Sala za Jioni za Kwaresma 2021