Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 27
Kushoto:
Umeonyesha nguvu kwa mkono wako
na kuwatawanya wenye kiburi katika mawazo ya
mioyo yao, Amewaangusha wakuu katika viti vya
vya enzi; na wayonge amewakweza.
Wenye njaa amewashibisha mema,
na matajari amewaondoa mikono mitupu.
Kulia:
Umemsaidia mtumishi wako, Israeli,
Ili kukumbuka rehema zake,
Kama alivyowaambia baba zake,
Ibrahimu na uzao wake hata milele.
Wote:
Atukuzwe Baba Mwana Roho Mtakatifu,
kama mwanzo, hata sasa, na siku zote hata
milele. Amina.
Mungu huwahurumia wale wamchao
Kizazi hata Kizazi.
Sala za waumini
Kiongozi:
Wote:
Kiongozi:
Wote:
Kiongozi:
Wote:
Yesu ulituonyesha jinsi ya kuwa wenye huruma,
kama vile Baba alivyo mwenye huruma;
Mioyo yetu, iliyofarijiwa na huruma ya Mungu,
iwe chemchemi za huruma kwa wote ambao
tunakutana nao katika safari ya maisha.
Yesu, ulitamani kufikia wote wenye changamoto
maishani, na tena uliwagusa wale ambao
walionekana kwamba ni wachafu.
Tuwezesha kushinda kila aina ya ubaguzi na
mitazamo maishani ili kusiwe na kizuizi kati
yetu na wale ambao wanahitaji huruma yetu.
Jibu lako, Yesu, kwa wote walioomba msaada wako
ilikuwa kusema, ndio nataka;
Jenga Kanisa lako kwa neema ile ile, kwamba
katika huu ulimwengu uliovunjika na wa
kutisha, litakuwa mahali penye huruma kwa
watu wote.
Wiki ya Nne - Jina la Mungu ni Huruma/Rehema
27