Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 29
Sala
Kiongozi:
Wote:
Ee Mungu, chemichemi cha kila humaru na wema
wote, tuangalie kwa neema.
Tunapoanza kipindi cha kwaresma
tuweze kuinuliwa daima na huruma yako.
Kwa njia ya Bwanao Yesu Kristo .
Amina
Baraka
Wote Tupige magoti
Kasisi / shemasi huenda kwenye altari, huinama na kupiga magoti. Wakati
wimbo unaozingatia Kristo unaimbwa, muhudumu, bado akipiga magoti,
huifukia ubani Sakramenti Kuu katika monstransi.Kisha anainuka na kusema:
Muhudumu:
Wote:
Tuombe:
Bwana Mungu wetu,
katika Sakramenti kuu hii
tunakuja mbele ya Yesu Kristo, Mwanao,
aliyezaliwa na Bikira Maria
na kusulubiwa kwa sababu ya wokovu wetu.
Siisi ambao tunatangaza imani yetu katika
chemchemi hii ya upendo na huruma, tunywa
kutoka kwake maji ya uzima wa milele.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu,
Amina
Baada ya sala muhudumu huvaa pazia la humeral, huinama na kuchukua monstransi. Kwa ukimya anawabariki watu kwa Ishara ya Msalaba na
monstransi. Sakramenti Kuu huchukuliwa kutoka kwa monstransi na kuekwa
katika Tebanako.
Mwisho
Kiongozi:
Wote:
Kiongozi:
Wote:
Wote wanasimama
Bwana awe nanyi
Awe pia nawe
Nendeni na amani ya Kristo
Tumshukuru Mungu.
Wiki ya Nne - Jina la Mungu ni Huruma/Rehema
29