Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 31
Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko
Wote waketi
‘.. uhusiano mzuri na maumile ni mwelekeo mmoja wa uongofu kwa
jumla, ambao unajumuisha kutambua makosa yetu, dhambi, hudhaifu
na kutofaulu, na kutuelekeza kwa Toba,na kuputa hamu ya mabadiliko
... “Ili kufikia upatanisho kama huo, lazima tuchunguze maisha yetu na
kutambua njia ambazo tumedhuru maumbile ya Mungu kupitia matendo
yetu na kushindwa kwetu kuchukuwa hatua. Tunahitaji kubadilika, au
kubadili mioyo. ” (Pope Francis, Laudato Sì, 218)
Tafakari
(Imetolewa na msemaji mgeni, kasisi, shemasi, waumini wa dini au walei)
Tafakari kwa kimya
Injili Takatifu: Somo (Lk 1:46-55)
Simameni
Kiongozi:
Wote:
nitatembea mbele yako, Ee Bwana,
maana njia zako ni kweli.
Kushoto:
Mwoyo wangu † wantukuza Bwana,
roho yangu inamshangilia Mungu Mwokozi
wangu;
kwa kuwa ameutamaza Unyonge wa Mjakazi
wake.
Kulia :
Kwa maana tazama tokea sasa vizazi wote
wataniita mbarikiwa. Kwa kuwa wenye Nguvu
amenitendea makuu,
na jina lako ni takatifu.
Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwa
hao wanamcha
Kushoto:
Umeonyesha nguvu kwa mkono wako
na kuwatawanya wenye kiburi katika mawazo ya
mioyo yao, Amewaangusha wakuu katika viti vya
vya enzi; na wayonge amewakweza.
Wiki ya tano - Katika Nyayo za Yesu
31