Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 34
Sala
Kiongozi:
Wote:
Mungu mwenye neema na upendo,
tunaomba kwamba, kwa msaada wako,
tuweza kutembea kwa hamu katika
njia ile ile ya upendo
ambayo Yesu alitembea duniani, hata hadi kifo.
Kwa nji ya Bwanao Yesu Kristo.
Amina
Baraka
Wote Tupige magoti
Kasisi / shemasi huenda kwenye altari, huinama na kupiga magoti.Wakati
wimbo unaozingatia Kristo unaimbwa, muhudumu, bado akipiga magoti,
huifukia ubani Sakramenti Kuu katika monstransi.
Kisha anainuka na kusema:
Muhudumu :
Wote:
Bwana Mungu wetu,
umetupa mkate wa kweli kutoka mbinguni.
Kwa nguvu ya chakula hiki
tuwejeshe tuishi daima kwa maisha yako
na kufufuka katika utukufu siku ya mwisho.
Tunaomba haya kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Amina
Baada ya sala muhudumu huvaa pazia la humeral, huinama na kuchukua
monstransi. Kwa ukimya anawabariki watu kwa Ishara ya Msalaba na
monstransi.
Sakramenti Kuu huchukuliwa kutoka kwa monstransi na kuekwa katika
Tebanako.
Mwisho
Kiongozi:
Wote:
Kiongozi:
Wote:
34
Wote wanasimama
Bwana awe nanyi
Awe pia na nafsi yako.
Nendeni kwa amani ya Kristo
Tumshukuru Mungu.
Sala za Jioni za Kwaresma 2021