Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 6
Evening Prayer
Every Week begins with pages 6-9
Mara tu watu wamekusanyika, kiongozi anwaalika wote wasimame.
Simameni
Kiongozi:
Ee Mungu, † njoo utusaidie
Wote:
Ee Bwana, fanya hima kwa msaada wako.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,
kama mwanzo, hata sasa, na milele yote . Amina.
Wimbo wa Kwaresima
Wakati wa wimbo Sakramenti Kuu imewekwa kwenye monstransi ambayo
huwekwa juu ya altari.
Zaburi
(Mistari ya zaburi husemwa kwa zamu na wale walio kwenye upande wa
kushoto na walio upande wa kulia)
Zaburi 33
6
Ketini wote
Kiongozi:
Wote:
Upendo wako uwe juu yetu, ee Bwana,
Tunapoweka matumaini yetu yote kwako
Kushoto:
Mpigieni Bwana vigelegele,enji wenye haki.
Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
Kulia:
Mshukuruni Bwana kwa kinubi,
Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe.
Kushoto:
Kwa kuwa neno la Bwana lina adili,
Na kazi yake yote huitanda kwa uamnifu.
Huzipenda haki na hukumu.
Nchi imejaa fadhili za Bwana.
Sala za Jioni za Kwaresma 2021