Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 7
Kulia:
Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika,
Na jeshi lake lote kwa punzi ya kinywa chake.
Hukusanya maji ya bahari chungu chungu,
Huviweka vilindi katika ghala.
Kushoto:
Nchi yote na imwogope Bwana,
Wote wakao duniani na wamche.
Maana yeye alisema, ikawa,
Na weye aliamuru ikasimama.
Kulia:
Heri taifa ambala Bwana ni Mungu wao,
Watu aliowachanguakuwa urithi wake.
Kutoka mbinguni Bwana hutazama,
Huwatazama wanadamu wote pia.
Kushoto:
Toka hahali pake aketipo,
Huwaangalia wote wakaao duniani,
Yeye aiumbaye mioyo yao yote huzifikiri kazi zao
zote.
Kulia:
Tazama jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojeao fadhili zake.
Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wake wa jaa.
Kushoto:
Nafsi zetu zinamngoja Bwana ,
yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Maana mioyo yetu itamfurahia ,
Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu.
Wote:
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,
kama mwanzo, hata sasa, na milele.
Amina.
Kiongozi:
Wote:
Upendo wako uwe juu yetu, ee Bwana,
Tunapokea matumaini yetu yote kwako
Kutakari kwa kimya
Zaburi
7