Sala za Jioni za Kwaresma 2021 SWAHILI - Book - Page 8
Zaburi 130
Kiongozi:
Wote:
Nafsi yangu inamngojea Bwana.
Na neno lake nimelitumainia
Kushoto:
Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia
Bwana, uisikia sauti yangu!
Masikio yako na yaisikilize
sauti ya dua zangu.
Kulia:
Bwana, kama wewe ungehesabu maovu,
Ee Bwana, nani angesimama?
Lakini kwako kuna msamaha:
Ili wewe uogopwe.
Kushoto:
Nimemngoja Bwana,
Royo yangu imengoja,
Naneno lake nimelitumainia
Nafsi yangu inangoja Bwana
Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,
Naam walinzi waingojao asubuhi.
Kulia:
Ee israeli umtarajie Bwana;
Maana kwa Bwana kuna fadhili,
Na kwake kuna ukobozi mwingi.
Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote.
Wote:
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,
kama mwanzo, hata sasa, na milele. Amina
Nafsi yangu inamngojea Bwana.
Na neno lake nimelitumainia
Kutakari kwa kimya
8
Sala za Jioni za Kwaresma 2021